JANUARI 14, 2019
MAMBO MAPYA
Tafsiri ya Ulimwengu Mpya Imetolewa Katika Lugha Tano
Januari 12, 2019, huko Benin City, Nigeria, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ilitolewa katika lugha ya Isoko na toleo lililorekebishwa la Tafsiri ya Ulimwengu Mpya lilitolewa katika lugha ya Yoruba. Siku hiyohiyo huko Dudley, West Midlands, Uingereza, kitabu cha Mathayo cha Tafsiri ya Ulimwengu Mpya kilitolewa katika Lugha ya Ishara ya Uingereza.
Tafsiri ya Ulimwengu Mpya pia ilitolewa katika lugha mbili nchini Filipino. Toleo lililorekebishwa lilitolewa katika lugha ya Cebuano Januari 12, 2019, katika jiji la Lapu-Lapu City, Cebu. Siku iliyofuata huko Palo, Leyte, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ilitolewa katika lugha ya Waray-Waray. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya imetafsiriwa ikiwa nzima au kwa sehemu katika lugha 179, kutia ndani lugha 18 zilizorekebishwa kulingana na toleo la 2013.