WIMBO NA. 49
Kufurahisha Moyo wa Yehova
-
1. Mungu nadhiri twaweka;
Kazi yako tutafanya.
Kufanya mapenzi yako
Hukufurahisha moyo.
-
2. ‘Mtumwako mwaminifu,’
Sifa zako hutangaza.
Anatulisha kiroho,
Ili tukutumikie.
-
3. Tupe roho takatifu,
Tuwe washikamanifu.
Tufanye uyapendayo,
Moyo wako ufurahi.
(Ona pia Mt. 24:45-47; Luka 11:13; 22:42.)