WIMBO NA. 139
Wazia Wakati Vitu Vyote Vitakuwa Vipya
-
1. Hebu waza, mimi nawe;
Sote katika dunia mpya.
Fikiria Paradiso,
Amani na uhuru tele,
Na uovu wote kwisha.
Utawala wake Yehova,
Utaitawala dunia yote.
Kwa moyo wote sote
tutamwimbia:
(KORASI)
“Yehova Mungu twakushukuru.
Umefanya vyote viwe vipya.
Tunachochewa na ukarimu wako;
Wastahili heshima na utukufu.”
-
2. Hebu waza, mimi nawe;
Tukiwa katika Paradiso.
Tuonayo, kusikia
Hayatatutia uoga.
Yote kweli, katabiri;
Hema lake kalitandaza,
Afufue walio kaburini;
Tumwimbie Yehova
sifa pamoja:
(KORASI)
“Yehova Mungu twakushukuru.
Umefanya vyote viwe vipya.
Tunachochewa na ukarimu wako;
Wastahili heshima na utukufu.”
(Ona pia Zab. 37:10, 11; Isa. 65:17; Yoh. 5:28; 2 Pet. 3:13.)