Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Marek M. Berezowski/Anadolu Agency via Getty Images

ENDELEA KUKESHA!

Vita Nchini Ukrainia Vyaingia Mwaka wa Pili—Biblia Inatoa Tumaini Gani?

Vita Nchini Ukrainia Vyaingia Mwaka wa Pili—Biblia Inatoa Tumaini Gani?

 Ijumaa, Februari 24, 2023, mwaka mmoja utakuwa umekwisha tangu jambo baya lilipotukia: vita nchini Ukrainia vilianza. Kulingana na ripoti fulani, wanajeshi 300,000 hivi wa Ukrainia na Urusi wamekufa au kujeruhiwa na inaaminiwa kwamba raia 30,000 hivi wamekufa katika vita hivyo. Hata hivyo, huenda idadi hizo zikawa juu zaidi.

 Kwa kusikitisha, haionekani kwamba vita hivyo vitakwisha hivi karibuni.

  •   “Karibu mwaka mmoja umepita tangu majeshi ya Urusi yalipoivamia Ukrainia na hakuna dalili zozote za kwamba vita hivi vitakwisha. Haionekani kama upande wowote utashinda vita hivi, wala haionekani kama pande zote zitakubaliana kuhusu utatuzi fulani.”​—NPR (National Public Radio), Februari 19, 2023.

 Inaeleweka kwa nini watu wengi wanahuzunishwa na maumivu na kuteseka ambako vita hivyo na vingine vingi ulimwenguni vimewasababishia watu wasio na hatia. Biblia inatoa tumaini gani? Je, kutakuwa na mwisho wa vita?

Vita vitakavyokomesha vita vyote

 Biblia inazungumza kuhusu vita vitakavyowaokoa wanadamu, si kuwaangamiza. Vita hivyo vinajulikana kama Har-Magedoni, na vinafafanuliwa kuwa “vita vya siku kuu ya Mungu Mweza-Yote.” (Ufunuo 16:14, 16) Mungu atatumia vita hivyo kukomesha utawala wa wanadamu, ambao umesababisha vita vingi sana vilivyotokeza uharibifu. Ili kujifunza jinsi Har-Magedoni itakavyoleta amani ya kudumu, soma makala zifuatazo: