Mimea Hutumiwa Kutengeneza Dawa
Mimea Hutumiwa Kutengeneza Dawa
Wataalamu wanakadiria kwamba robo ya dawa zote ambazo watu hutumia leo zimetengenezwa moja kwa moja kutokana na mimea au kwa kutumia sehemu fulani za mimea. Mara nyingi, watetezi wa mitishamba hutaja jambo hilo.
Utafiti mwingi hufanywa kuhusu mimea inayotengeneza dawa ili kupata kemikali za dawa. Mfano mzuri ni aspirini inayotengenezwa kutokana na salicin, ambayo hutolewa kwenye gamba la mti unaoitwa willow.
Kemikali hizo zinaweza kutumiwa kwa kiwango kinachofaa baada ya kutolewa kwenye mmea. Kitabu kimoja kinasema: “Ni rahisi kumeza tembe ya aspirini au ya digitalis kuliko kutumia magamba mengi ya mti wa willow au mimea mingi ya foxglove.”
Kwa upande mwingine, kuna hasara za kutoa kemikali muhimu kutoka kwa mmea. Kwa kufanya hivyo sehemu nyingine za mmea zinazoweza kuliwa au kutumiwa katika matibabu zinaweza kupotea bure. Isitoshe, viini fulani vinavyosababisha magonjwa vimeanza kukinza dawa.
Mfano mmoja wa hasara za kutoa kemikali muhimu kutoka kwa mmea ni wa kwinini, ambayo inapatikana kwenye gamba la mti wa cinchona. Ijapokuwa kwinini hiyo huua viini vingi vya malaria, viini vinavyosalia huongezeka. Kitabu kimoja kinaeleza: “Wataalamu wa tiba wanahangaikia sana suala la viini sugu.”
[Picha katika ukurasa wa 15]
Aspirini hutolewa kwenye mti wa “willow”
[Hisani]
USDA-NRCS PLANTS Database/Herman, D.E. et al. 1996. North Dakota tree handbook
[Picha katika ukurasa wa 15]
Kwinini hutolewa kwenye mti wa “cinchona”
[Hisani]
Courtesy of Satoru Yoshimoto