Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 14. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Ni nani aliyewaficha manabii 100 wa Yehova katika mapango, wakati Yezebeli alipoamuru wauawe? (1 Wafalme 18:3, 4)

2. Ni jina gani la cheo la Yesu lililojulikana hata kwa roho mwovu asiye safi wakati Yesu alipomfukuza roho huyo kutoka kwa mtu katika sinagogi huko Kapernaumu? (Luka 4:34)

3. Mume wa Naomi aliitwa nani? (Ruthu 1:3)

4. Ni watawala gani watano wa Roma waliotajwa na Luka ili kutambulisha wakati ambapo Yohana Mbatizaji alianza huduma yake? (Luka 3:1)

5. Milango ya hekalu na ya tabenakulo ilifunguka kuelekea upande gani? (Hesabu 3:38)

6. Yese alikuwa na wana wangapi, na Daudi alikuwa mwana wa ngapi? (1 Samweli 17:12, 14)

7. Kwa nini Mafarisayo walimuuliza Yesu maswali? (Mathayo 22:15)

8. Samsoni alienda kwenye jiji gani la Wafilisti ili kupata mavazi 30 ya kuwapatia wale ‘waliokitambua’ kitendawili chake? (Waamuzi 14:19)

9. Katika njozi ya Yohana inayohusu kiti cha enzi cha Yehova, kiumbe hai wa pili alifanana na nini? (Ufunuo 4:7)

10. Ni jiji gani ambalo Yehova hakuliharibu wakati mfalme na watu wake walipotubu uovu wao? (Yona 3:1-10)

11. Kwa nini tunashauriwa kuwa “watiifu kwa wale ambao wanaongoza” katika kutaniko? (Waebrania 13:17)

12. Ni nabii yupi aliyetabiri kwamba “wale ambao si watu wangu hakika nitawaita ‘watu wangu,’” aliposema jinsi ambavyo Mungu angewakataa Waisraeli wa asili na kukubali taifa la kiroho? (Waroma 9:25)

13. Katika njozi ya Yohana, malaika anatumia nini kumfunga Shetani? (Ufunuo 20:1)

14. Kwa nini Akila na Prisila walihama Roma na kwenda Korintho? (Matendo 18:2)

15. Kwa nini hasira ya Mungu haina makosa? (Yoshua 7:1)

16. Isaya aliwafananisha na nini watu waovu waliotengwa na Mungu? (Isaya 57:20)

17. Ni nani aliyekuwa mfalme wa mwisho wa Yuda kutawala katika Yerusalemu? (2 Wafalme 24:18)

18. Yesu alimwambia nini mwandishi aliyesema angemfuata popote ambapo angeenda, akionyesha kwamba wale ambao wangemfuata wangepatwa na magumu? (Luka 9:58)

19. Ni mfalme yupi mwovu wa Moabu aliyekuwa na tumbo kubwa sana hivi kwamba Ehudi alipomchoma tumboni, upanga wote ulizama ndani? (Waamuzi 3:17-22)

20. Kleopasi alimuuliza Yesu swali gani, akionyesha mshangao kwa sababu aliona kwamba Yesu hakujua mambo yaliyokuwa yametukia majuzi huko Yerusalemu? (Luka 24:18)

Majibu kwa Maswali

1. Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba ya mfalme

2. “Mtakatifu wa Mungu”

3. Elimeleki

4. Tiberio Kaisari, Pontio Pilato, Herode Antipasi, Filipo ndugu yake, na Lisaniasi

5. Mashariki

6. Wanane, mdogo wa wote

7. “Kusudi wamtege katika usemi wake”

8. Ashkeloni

9. “Fahali mchanga”

10. Ninawi

11. Ili waweze kutoa hesabu yao “kwa shangwe na si kwa kutweta,” jambo ambalo lingekuwa lenye “hasara” kwetu

12. Hosea

13. “Mnyororo mkubwa”

14. Kwa sababu Klaudio aliwaagiza Wayahudi wote waondoke Roma

15. Wakati wote hiyo ni ya haki, imedhibitiwa, na inapatana na sifa zake za upendo, hekima, na haki

16. Bahari iliyochafuka

17. Sedekia

18. “Mwana wa binadamu hana mahali popote pa kulaza kichwa chake”

19. Egloni

20. “Je, wewe unakaa peke yako kama mgeni wa nchi nyingine katika Yerusalemu?”