Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Milford Sound

NCHI NA WATU

Kutembelea New Zealand

Kutembelea New Zealand

MIAKA 800 hivi iliyopita, Wamaori walisafiri maelfu ya kilometa baharini na kuhamia New Zealand. Waligundua kwamba nchi hiyo ilikuwa yenye milima na miamba ya barafu, na vilevile chemchemi za maji moto na theluji, tofauti na visiwa vyenye joto vya Polinesia, mahali walikotoka. Wahamiaji wengine waliwasili miaka mia tano hivi baadaye, wakitokea Ulaya. Leo, wenyeji wengi wa New Zealand wanafuata tamaduni za Waingereza wenye asili ya Ujerumani na Wapolinesia. Karibu asilimia 90 ya wakazi nchini humo wanaishi mjini. Jiji la Wellington ni la pekee kwa sababu ndio mji mkuu ulio mwishoni zaidi kusini mwa dunia.

Madimbwi ya matope yanayotokota katika Kisiwa cha Kaskazini

Kwa kuwa New Zealand ina mandhari mbalimbali zenye kupendeza, haishangazi kwamba watalii milioni tatu hivi hutembelea nchi hiyo kila mwaka licha ya kuwa imejitenga.

Mkangaga wenye rangi ya fedha unaweza kukua na kufikia kimo cha mita 10 au zaidi

Hadi kufikia mwaka wa 1948, ndege asiyepaa anayeitwa takahe alidhaniwa kuwa ametoweka

New Zealand inajivunia kuwa na wanyama pori wa pekee, ikiongoza kwa kuwa na aina nyingi za ndege wasiopaa kuliko eneo lingine lolote duniani. Pia, mnyama jamii ya mjusi anayeitwa tuatara, aliye na uwezo wa kuishi hadi miaka 100, anapatikana nchini humo! Wanyama pekee jamii ya mamalia walio na asili ya nchi hiyo ni aina fulani ya popo na baadhi ya viumbe wakubwa wa baharini, wanaotia ndani nyangumi na pomboo.

Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakihubiri nchini New Zealand kwa karibu miaka 120. Wao hufundisha Biblia katika lugha 19 hivi, kutia ndani lugha za Kipolinesia, kama vile Kiniue, Kirarotonga, Kisamoa, na Kitonga.

Wamaori wakiimba kwa mpangilio wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni