Pasaka—Inawahusuje Wakristo
Ili Waisraeli wasipate madhara ya pigo la kumi, ilikuwa muhimu kwao kutii maagizo. (Kut 12:28) Usiku wa Nisani 14, familia zilipaswa kukusanyika ndani ya nyumba zao. Walipaswa kumchinja mwanakondoo au mbuzi asiye na kasoro mwenye umri wa mwaka mmoja. Damu yake ilipaswa kunyunyizwa kwenye miimo ya mlango na kwenye kizingiti cha juu ya mlango. Walipaswa kuchoma nyama yote na kuila haraka. Hakuna aliyepaswa kutoka nje ya nyumba mpaka asubuhi.—Kut 12:9-11, 22.
Ni katika njia zipi hususa utii unatulinda leo?