Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Januari 15-21

AYUBU 36-37

Januari 15-21

Wimbo 147 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Kwa Nini Unaweza Kuamini Ahadi ya Mungu ya Uzima wa Milele

(Dak. 10)

Yehova mwenyewe anaishi milele (Ayu 36:26; w15 10/1 13 ¶1-2)

Yehova ana hekima na nguvu za kuendeleza uhai (Ayu 36:​27, 28; w20.05 22 ¶6)

Yehova anatufundisha jinsi tunavyoweza kupata uzima wa milele (Ayu 36:​4, 22; Yoh 17:3)


Imani yenye nguvu katika ahadi ya Mungu ya uzima wa milele inatuimarisha na kutusaidia kukabiliana na hali ngumu maishani.—Ebr 6:19; w22.10 28 ¶16.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Ayu 37:20—Mara nyingi habari ziliwasilishwa kwa njia gani katika maeneo yanayotajwa katika Biblia? (it-1 492)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) MAHUBIRI YA UMMA. (lmd somo la 3 jambo kuu la 3)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 4) NYUMBA KWA NYUMBA. (lmd somo la 2 jambo kuu la 5)

6. Kufafanua Imani Yako

(Dak. 5) Hotuba. ijwfq 57 ¶5-15—Kichwa: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Waliteswa Wakati wa Yale Maangamizi Makubwa ya Wanazi? (th somo la 18)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 49

7. Jitayarishe Kushughulikia Hali za Kiafya Zinazohitaji Matibabu au Upasuaji

(Dak. 15) Mazungumzo. Yaongozwe na mzee.

Tengenezo la Yehova limetuandalia vifaa vya kutusaidia kutii sheria ya Mungu kuhusu damu. (Mdo 15:​28, 29) Je, unavitumia vizuri?

Kadi ya Mamlaka ya Kudumu ya Uwakilishi (DPA) na Kadi ya Utambulisho (ic): Kadi hizo zinaonyesha maamuzi ya mgonjwa kuhusu matumizi ya damu katika matibabu. Wahubiri waliobatizwa wanaweza kujipatia kadi ya DPA na Kadi ya Utambulisho kwa ajili ya watoto wao kutoka kwa mtumishi wa machapisho. Tunapaswa kubeba kadi hizo nyakati zote. Ikiwa unahitaji kujaza kadi mpya au kujaza habari za karibuni, usiahirishe.

Habari kwa Akina Mama Wajawazito (S-401) na Habari kwa Ajili ya Wagonjwa Wanaohitaji Upasuaji au Matibabu ya Mionzi (S-407): Fomu hizo zinatusaidia kujitayarisha vizuri kwa ajili ya matibabu tunayohitaji, kutia ndani mambo yanayohusu suala la damu. Waombe wazee wa kutaniko lako nakala ya fomu unayohitaji ikiwa wewe ni mja-mzito au unahitaji kufanyiwa upasuaji au matibabu ya kansa.

Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali (HLC): Washiriki wa HLC ni wazee wanaostahili na waliozoezwa kuwapa madaktari na wahubiri habari kuhusiana na damu. Wanaweza kuzungumza na daktari wako kuhusu mbinu za matibabu za kuepuka kutiwa damu mishipani. Ikihitajika, wanaweza kukusaidia kupata daktari atakayeheshimu maamuzi yako. Ndugu hao wanapatikana saa 24, kila siku ya juma. Wasiliana na HLC haraka iwezekanavyo kuhusu hali yoyote ambayo huenda ikahitaji ulazwe hospitalini, kufanyiwa upasuaji, au matibabu ya kuendelea—kama vile matibabu ya kansa—hata ikiwa inaonekana kwamba suala la damu halitahusika. Hilo linawahusu pia akina mama waja-wazito. Ikiwa unahitaji msaada, mwombe mzee habari za mawasiliano ya HLC.

Onyesha VIDEO Halmashauri za Uhusiano na Hospitali—Zinasaidiaje? Kisha uwaulize wasikilizaji:

HLC inaweza kukusaidiaje unapohitaji matibabu au upasuaji?

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 67 na Sala