Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

Yehova Anawapanga Watu Wake

Yehova Anawapanga Watu Wake

[Onyesha video yenye kichwa Utangulizi wa Hesabu.]

Waisraeli walipiga kambi kulingana na makundi ya makabila matatu (Hes 1:52, 53; w94 12/1 9 ¶4)

Huenda kambi yote ya Waisraeli ilikuwa na jumla ya watu 3,000,000 au zaidi (Hes 2:32, 33; it-1 397 ¶4)

Yehova anataka watu wake wamwabudu kwa mpango. Taifa la Israeli lilimwabudu hivyo, nasi tunamwabudu vivyo hivyo leo.—1Ko 14:33, 40.

Mwonekano wa mpangilio wa kambi ya Waisraeli. Hema la ibada liko katikati. Karibu na hema la ibada kulikuwa na familia za kabila la Walawi: Haruni upande wa mashariki, Wakohathi upande wa kusini, Wagershoni upande wa magharibi, na Wamerari upande wa kaskazini. Makabila 12 ya Waisraeli yako mbali zaidi. Upande wa mashariki kuna kabila la Isakari, Yuda, na Zabuloni. Upande wa kusini kuna kabila la Gadi, Rubeni na Simeoni. Upande wa magharibi kuna kabila la Benjamini, Efraimu, na Manase. Upande wa kaskazini kuna kabila la Naftali, Dani, na Asheri.

JIULIZE, ‘Ninaweza kuonyeshaje kwamba ninaunga mkono tengenezo la Yehova kikamili?’