JULAI 22, 2024
URUSI
Ndugu Valeriy Baylo Amehukumiwa Kifungo cha Gerezani
Julai 3, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Abinskiy iliyo katika Eneo la Krasnodar ilimhukumu Ndugu Valeriy Baylo kifungo cha miaka miwili na miezi sita gerezani. Kwa kuwa tayari alikuwa gerezani ataendelea kubaki huko.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwaandalia Valeriy na ndugu na dada zetu wote walio gerezani ulinzi kwa “upendo [wake] wa milele.”—Yeremia 31:3.
Mfuatano wa Matukio
Machi 28, 2024
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Aprili 2, 2024
Alihojiwa na kushtakiwa kuwa mhalifu kwa kushiriki utendaji wa shirika lenye msimamo mkali. Akawekwa kizuizini
Aprili 4, 2024
Alipelekwa mahabusu ili kusubiri hukumu
Juni 26, 2024
Kesi ya uhalifu ilianza
Julai 3, 2024
Baada ya kusikiliza kesi yake mara tatu tu, hakimu alimhukumu Valeriy kifungo cha miaka miwili na miezi sita gerezani