OKTOBA 8, 2020
URUSI
Mahakama ya Urusi Yahukumu Wenzi wa Ndoa Wenye Umri Mdogo, Yawapa Vifungo vya Nje
Oktoba 8, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Zasviyazhsky ya Jiji la Ulyanovsk iliwahukumu Ndugu Aleksandr Ganin, Khoren Khachikyan, Ndugu Andrey Tabakov, na Ndugu Mikhail Zelenskiy, kutia ndani Sergey Mysin na mke wake, Nataliya. Wote walipewa vifungo vya nje vya kuanzia miaka miwili na miezi sita hadi miaka minne. Hilo linamaanisha kwamba ndugu na dada hao hawatahitaji kwenda gerezani wakati huu.