FEBRUARI 9, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kimbunga Ana Kinapiga Eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika
Januari 24 hadi 25, 2022, mafuriko na upepo mkali ulioletwa na Kimbunga Ana vilisababisha uharibifu mkubwa nchini Malawi na Msumbiji. Kimbunga hicho kilisababisha vifo vya watu wengi, kikaharibu barabara, na nyumba, na hivyo kuwaacha maelfu ya watu bila makao.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Malawi
Inasikitisha kwamba ndugu mmoja alipoteza mke wake ambaye si Shahidi pamoja na watoto wao wawili, wenye umri wa miaka 3 na 5, walipozama baada ya mashua iliyokuwa ikiwaokoa kupinduka
Dada 1 alijeruhiwa. Msichana mwenye umri wa miaka 7 ambaye ni mtoto wa Mashahidi alijeruhiwa pia
Wahubiri 1,000 hivi wamelazimika kuhama makao yao
Majumba 2 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Nyumba 100 hivi zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 100 hivi ziliharibiwa kabisa
Msumbiji
Hakuna ndugu au dada aliyekufa
Ndugu 2 walijeruhiwa
Wahubiri 381 walilazimika kuhama makao yao
Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mkubwa
Majumba 3 ya Ufalme yaliharibiwa kabisa
Nyumba 51 zilipata uharibifu mdogo
Nyumba 96 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 79 ziliharibiwa kabisa
Jitihada za Kutoa Msaada
Halmashauri za Kutoa Msaada (DRC) zimeundwa katika nchi zote mbili
Halmashauri hizo zinaandaa chakula, maji safi ya kunywa, na mahitaji mengine
Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda na COVID-19
Tuna uhakika kwamba Yehova atawaimarisha ndugu zetu wakati huu wa taabu.—Zaburi 46:1.