SEPTEMBA 4, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: JANUARI 14, 2025
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEFUNGWA | Kuimarisha Imani Ili Kushinda Woga
Januari 14, 2025, Mahakama ya Wilaya ya Gagarinskiy iliyo Sevastopol, Crimea, iliwahukumu Viktor Kudinov na Ndugu Sergey Zhigalov kifungo cha miaka sita gerezani kila mmoja. Walipelekwa gerezani moja kwa moja baada ya kutoka mahakamani.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Yehova ni Mungu “anayefurahia amani ya [watumishi] wake.” Kwa hiyo, tuna uhakika kwamba ataendelea kuwabariki Viktor na Sergey kwa sababu wanaonyesha subira na uvumilivu.—Zaburi 35:27.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 24, 2022
Kesi ya uhalifu yafunguliwa. Nyumba zao zafanyiwa msako. Wanakamatwa na kuwekwa kizuizini
Agosti 26, 2022
Wanaachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Oktoba 17, 2022
Wanaachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vingine
Aprili 13, 2023
Kesi ya uhalifu yaanza