NOVEMBA 12, 2020
FILIPINO
Vimbunga Viwili Vyashambulia Maeneo Mengi Nchini Filipino
Mahali
Kusini mwa Luzon na visiwa vinavyoizunguka
Janga
Oktoba 25, 2020, Kimbunga Molave, kilichoitwa pia Quinta nchini Filipino kilipiga kijiji cha Albay kilicho katika mkoa wa Bicol ulio Luzon, Filipino. Upepo huo mkali ulivuma katika kisiwa chote cha Luzon
Novemba 1, 2020, Kimbunga Goni kilichokuwa na kasi sana, kilipewa jina Rolly nchini Filipino, kilipiga kisiwa cha Catanduanes katika mkoa wa Bicol ulio Luzon. Kimbunga hicho kiliendelea kuvuma hadi kwenye vijiji vingine, hadi vile ambavyo vilikuwa vimeathiriwa na Kimbunga Molave
Vimbunga hivyo viwili vilileta mvua kubwa na upepo mkali ambao ulisababisha mafuriko makubwa pamoja na ukosefu wa umeme na maji. Kuwasiliana na watu walio katika maeneo hayo ni vigumu sana
Mvua hizo kubwa zimesababisha pia lahars au matope yanayokuja na mabaki ya volcano ya Mlima Mayon ambayo yameharibu nyumba za watu wanaoishi karibu na mlima huo.
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Wahubiri wengi wamepoteza makao au kulazimika kuhama makao yao
Dada mwenye umri wa miaka 89 alijeruhiwa kidogo alipokuwa akikimbia kutoka katika nyumba yake ambayo iliharibiwa kabisa
Uharibifu wa mali
Nyumba 134 na Majumba ya Ufalme 8 yalipata uharibifu mkubwa
Nyumba 75 na Majumba ya Ufalme 8 yaliharibiwa kwa kadiri ndogo
Nyumba 101 na Jumba ya Ufalme 1 liliharibiwa kabisa
Jitihada za kutoa msaada
Waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa wanashirikiana na Halmashauri 6 za Kutoa Msaada ili akina ndugu wapate chakula, maji, mahali pa kuishi na mahitaji mengine ya lazima. Ndugu zetu wanafuata kwa makini miongozo ya jinsi ya kujilinda na ugonjwa wa COVID-19
Tutaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu ambao wameathiriwa na majanga haya ya asili. Katika kipindi hiki kigumu, tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwa “Baba wa rehema nyororo na Mungu wa faraja yote” kwa ndugu na dada zetu.—2 Wakorintho 1:3.