JANUARI 20, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 19, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAPIGWA FAINI | Ndugu Saba Nchini Urusi Wanamtegemea Yehova Anayewapa Nguvu
Desemba 17, 2024, Mahakama ya Jiji la Pechora katika Jamhuri ya Komi iliwahukumu Ndugu Nikolay Anufriyev, Ndugu Eduard Merinkov, Ndugu Gennadiy Polyakevich, Ndugu Aleksandr Prilepskiy, Ndugu Viktor Shchannikov, Ndugu Gennadiy Skutelets, na Ndugu Aleksandr Vorontsov. Ndugu sita kati yao walitozwa faini. Nikolay, Eduard, Viktor, na Aleksandr Vorontsov walitozwa faini ya rubo 600,000 (dola 5,797.00 za Marekani); Gennadiy Skutelets alitozwa faini ya rubo 250,000 (dola 2,413.00 za Marekani); na Gennadiy Polyakevich alitozwa faini ya rubo 200,000 (dola 1,931.00 za Marekani). Aleksandr Prilepskiy alihukumiwa kuwa na hatia, lakini kesi hiyo ilifutiliwa baada ya kifo chake mwezi Desemba 2022.
Mfuatano wa Matukio
Januari 28, 2020
Wenye mamlaka walifanya msako katika nyumba za familia 12 za Mashahidi wa Yehova katika Jamhuri ya Komi. Kesi ya uhalifu dhidi ya Ndugu Polyakevich na Ndugu Skutelets ilianzishwa
Januari 30, 2020
Gennadiy Polyakevich alipelekwa mahabusu na Gennadiy Skutelets alifungwa kifungo cha nyumbani
May 20-25, 2020
Wenye mamlaka waliwahoji akina ndugu na dada wengine kutoka Pechora ili waone ikiwa wangewatumia kama mashahidi katika kesi hiyo ya uhalifu. Ndugu mmoja alipatwa na ugonjwa wa kiharusi baada ya kutishwa na mpelelezi mmoja. Sasa amepata nafuu
Juni 26, 2020
Muda wa Gennadiy Polyakevich kukaa mahabusu uliongezwa. Hakimu alisema kwamba Gennadiy Polyakevich anashtakiwa kwa “kutenda kimakusudi uhalifu mkubwa,” unaotia ndani kuzungumza kuhusu “umuhimu wa kuendelea kumtumikia Yehova licha ya kuteswa na wenye mamlaka.”
Agosti 24, 2020
Wenye mamlaka walifanya msako katika nyumba za familia nyingine 12 za Mashahidi
Novemba 10, 2020
Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Aleksandr Prilepskiy, Aleksandr Vorontsov, Eduard, Nikolay, na Viktor. Kesi hiyo iliunganishwa na kesi ya uhalifu dhidi ya Gennadiy Polyakevich na Gennadiy Skutelets
Novemba 25, 2020
Baada ya kukaa mahabusu siku 300, Gennadiy Polyakevich aliachiliwa kisha akafungwa kifungo cha nyumbani
Januari 27, 2021
Baada ya kuwa katika kifungo cha nyumbani kwa siku 363, Gennadiy Skutelets aliachiliwa
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tuna uhakika kwamba ndugu zetu walio na imani katika wema wa Yehova watabarikiwa sasa na wakati ujao pia.—Zaburi 27:13.