AGOSTI 16, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 5, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—UAMUZI WAPINDULIWA | “Sisi Sote Ni Kitu Kimoja”
Desemba 5, 2023, Mahakama ya Eneo la Khabarovsk ilibadili hukumu dhidi ya Dada Lyubov Kocherova na Dada Lyubov Ovchinnikova. Kesi yao sasa itarudishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Khabarovskiy ya Eneo la Khabarovsk ili isikilizwe upya.
Agosti 1, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Khabarovskiy iliyo katika Eneo la Khabarovsk iliwahukumu Dada Lyubov Kocherova na Dada Lyubov Ovchinnikova kifungo cha nje cha miaka sita kila mmoja. Hawatahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Masimulizi ya ndugu na dada wanaoendelea kubaki waaminifu licha ya mateso yanatukumbusha kwamba Yehova ni mwenye upendo na “[anawapa] wote nguvu.”—1 Mambo ya Nyakati 29:12.
Mfuatano wa Matukio
2019-2020
Wenye mamlaka walianza kurekodi kisiri mazungumzo ya dada hao
Machi 3, 2022
Msako ulifanywa kwenye nyumba ya dada Lyubov Kocherova. Walichukua simu yake na pia kompyuta yake
Mei 26, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Lyubov Kocherova
Mei 28, 2022
Lyubov Kocherova alihojiwa
Novemba 7, 2022
Kesi ya uhalifu yafunguliwa dhidi ya Lyubov Ovchinnikova. Kesi hizo mbili ziliunganishwa na kuwa kesi moja
Januari 21, 2023
Msako wafanywa tena katika nyumba ya Lyubov Kocherova
Aprili 25, 2023
Kesi ya uhalifu yaanza